Juhudi za Fasihi katika Kukabiliana na Janga la 'UKIMWI'
Kifani cha Riwaya ya 'Ua la Faraja'
Keywords:
UKIMWI, Fasihi, Afya, JangaAbstract
Janga la UKIMWI (Ukosefu wa Kinga Mwilini) limekuwa katika bara la Afrika kwa muda sasa. Licha ya kuzuka kwa majanga mengine ya kiafya kama saratani, korona, kisukari miongoni mwa mengine, UKIMWI bado unatishia kudumaza mustakabali wa bara Afrika. Hali hii inatokana na maambukizi yake kusambaa na kuongezeka kila uchao. Mikakati kadhaa imewekwa na Shirika la Afya Duniani (World Health Organization-WHO) ikiwemo kuwaelimisha watu kuepuka maambukizi ya ugonjwa huu kama hatua ya kukabiliana nao. Fasihi ni mojawapo katika nyenzo hizi zinazotumiwa kufundisha na kuielekeza jamii. Ni kwa misingi hii ambapo makala haya yamezuumu kudadisi na kutathimi mchango wa fasihi ya Kiswahili katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Makala haya yanahakiki riwaya ya Ua la Faraja (2004). Uteuzi wa riwaya hii ulifanywa kimakusudi kutokana na upekee wake wa kuliangazia janga hili kwa mapana. Makala haya hivyo basi yanachunguza namna mwandishi anavyosawiri ugonjwa huu tangu ulipochipuka duniani, namna unavyoambukizwa, athari zake kwa umma na jinsi ya kuepuka maambukizi yake. Mwisho, makala yanadhihirisha kuwa licha ya hatari inayoletwa na ugonjwa huu, yapo matumaini makubwa katika udhibiti wake barani Afrika.