Uteuzi wa Lugha katika Mahubiri ya Kikristo Jijini Nairobi

Authors

  • Alex Umbima Kevogo Chuo Kikuu cha Garissa Author
  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Mahubiri, Muktadha, Wingilugha, Lugha

Abstract

Makala haya yalichunguza hoja zilizoathiri uteuzi wa lugha iliyotumiwa na wahubiri wa Kikristo jijini Nairobi katika mahubiri yao. Wahubiri kadha kutoka kwa makanisa mbalimbali walishirikishwa katika utafiti huu. Wahubiri hao walihitajika kujaza hojaji na vilevile kushiriki kwenye mahojiano ya ana kwa ana wakati wa kukusanya data. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa hoja zilizoathiri uteuzi wa lugha katika mahubiri ya Kikristo jijini Nairobi ni pamoja na: aina ya washiriki katika mazungumzo, muktadha wa mazungumzo, yaliyomo kwenye mazungumzo, uamilifu wa mazungumzo na malengo ya mazungumzo. Aidha, tuligundua kuwa wahubiri wa Kikristo jijini Nairobi waliteua lugha ya kutumia katika mahubiri wakizingatia jukumu mahususi ambalo lingetekelezwa na lugha iliyoteuliwa kufanikisha malengo yao ya Kimawasiliano. Utafiti unabainisha umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika kufanikisha mawasiliano ya kidini katika maeneo yaliyo na sifa ya wingilugha.

Downloads

Published

30-04-2021

Issue

Section

Articles