About the Journal

Mwanga wa Lugha ni jarida la Idara ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret-Kenya. Jarida hili huchapisha makala za lugha, isimu na fasihi. Aidha, jarida hili huchapishwa mara mbili kwa mwaka, yaani Aprili na Septemba.

Maelekezo kwa Waandishi wa Makala

Waandishi wanaombwa kuwasilisha makala zao kwa kuzingatia maagizo yafuatayo:

  1. Makala yawe na kichwa, jina la mwandishi, chuo, taasisi au shirika analofanyia kazi, anwani ya posta na barua pepe, nambari ya simu na taarifa fupi kuhusu mwandishi. Taarifa hizi zitokee kwenye ukurasa wa kwanza.
  2. Makala yapigwe chapa kwa kutumia programu ya MS WORD, kwa kuzingatia utaratibu wa Times New Roman kwenye umbo la A4, kukiwa na nafasi ya 1.5 baina ya mistari na maandishi yawe ni ya kiwango cha 12.
  3. Ikisiri iandikwe kwa kutumia italiki, isizidi maneno 200 na itokee mwanzoni mwa makala, chini ya taarifa zilizotajwa hapo juu (1).
  4. Idadi ya maneno isizidi 6000 na isipungue 3500.
  5. Lugha ya jarida iwe ni Kiswahili tu. Hata hivyo makala yaliyoandikwa kwa Kiingereza yanaweza kufikiriwa.
  6. Marejeleo yaandikwe kwa kutumia mfumo wa APA.
  7. Ikiwa ni lazima mwandishi atumie tanbihi, tunapendekeza matumizi ya tanbihi mwisho badala ya tanbihi chini.

 

Wasiliana nasi Kupitia:

Ama

Mhariri Mkuu

Jarida la Mwanga wa Lugha

Idara ya Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika

Chuo Kikuu cha Moi

S.L.P 3900-30100

Eldoret-Kenya.

 

Au

Jaridalamwangawalugha@gmail.com na jaridalamwangawalugha@mu.ac.ke