Mchango wa Kazi Teule za Fasihi katika Kukabiliana na Janga la UKIMWI

Authors

  • Charles Kituni Wasike Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi Author
  • S. M. Obuchi Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Maradhi, Dhamira, UKIMWI, Unyanyapaa

Abstract

Janga la UKIMWI limekuwa katika jamii zetu kwa zaidi ya miaka thelathini. Katika kipindi hicho zaidi ya watu milioni 34 wameambukizwa ugonjwa huo ulimwenguni. Isitoshe, kwa mujibu wa UNAIDS (2012), zaidi ya watu milioni 18 wameaga dunia. Tangu kisa cha kwanza cha UKIMWI kugunduliwa nchini Kenya, juhudi mbalimbali zimefanywa kujaribu kupunguza idadi ya visa vya maambukizi mapya. Juhudi hizo ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu mbinu na njia mbalimbali za kujikinga dhidi ya maambukizi. Njia moja muhimu ambayo yaweza kutumiwa kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu UKIMWI ni kupitia kazi ya fasihi. Kwa mintarafu hiyo, makala haya hususan yanatathmini mchango wa kazi teule za fasihi andishi katika kukabiliana na janga la UKIMWI. Kwa vile tiba ya UKIMWI haijagunduliwa, utafiti huu ulilenga kutoa mchango kwa jamii ambao waweza kufahamisha umma kuhusu mbinu na njia za kutumika katika kukabiliana na janga la UKIMWI.

Downloads

Published

30-09-2019

Issue

Section

Articles