Tathmini ya Mikakati ya Tafsiri ya 'Vinay na Derbelnet' (2004) katika Tafsiri ya 'A Good Day' (2019)
Keywords:
Mikakati ya Tafsiri, Siku Njema, A Good DayAbstract
Uteuzi wa mikakati ya tafsiri katika mchakato wa tafsiri, ni suala muhimu katika Nadharia ya Tafsiri. Lengo la makala haya ni kutathmini mikakati ya tafsiri iliyotumiwa katika kutafsiri ya riwaya ya Kiswahili Siku Njema iliyotafsiriwa kwenda Kiingereza kama A Good Day. Uteuzi wa mikakati ya tafsiri unaweza kuwa na athari zake katika uhawilishaji wa ujumbe. Hata hivyo, suala hili halijapewa nafasi inayostahiki katika tafiti tangulizi kuhusu kazi za tafsiri. Tathmini za tafsiri hujikita kuchanganua changamoto za tafsiri bila kuonesha kwamba uteuzi wa mikakati ya tafsiri una mchango mkubwa katika kuibua changamoto hizo. Modeli ya Vinay na Derbelnet (2004) ilitumiwa kubaini mikakati ya tafsiri iliyotumiwa na wafasiri Dorothy Kweyu na Fortunatus Kawegere. Wataalamu wanakubaliana kwamba Modeli ya Vinay na Derbelnet ndio msingi wa uainishaji wa mikakati ya tafsiri na wataalamu wengine wanaoainisha mikakati ya tafsiri hutumia modeli hii kama msingi wa uainishaji wao.