Uchanganuzi wa Mtindo katika Sajili ya Vyombo vya Habari
Keywords:
Vyombo vya Habari, Mawasiliano, Sajili, MtindoAbstract
Lugha, kama malighafi ya vyombo vya habari, huwezesha na kufanikisha mawasiliano miongoni mwa wanajamii. Tunapozungumzia mawasiliano tunazungumzia utumaji na upokeaji wa jumbe mbalimbali. Ni jumbe zinazojengwa kupitia lugha. Kwa hivyo, suala la uamilifu wa lugha linajitokeza. Ni kupitia utendaji kazi wa lugha ambapo tunaibuka na sifa za kitaaluma na za kisajili. Katika makala haya tunashughulikia sajili ya vyombo vya habari. Kipengele cha sajili ni zao la miktadha mbalimbali ya mawasiliano. Makala haya yanachanganua mtindo katika muktadha wa mawasiliano ya vyombo vya habari kiusemi, kiuandishi na kielektroniki. Sifa za kimtindo hutegemea iwapo ni taarifa ya habari, michezo ya kuigiza, matangazo ya kibiashara n.k. Makala yanadhihirisha kuwa kuna mitindo anuwai katika mawasiliano ya kiuandishi. Ni mitindo inayoendelea kubuniwa na kupanuka kadri ya mpito wa wakati.