Ushairi wa Mnyampala kama Hifadhi ya Historia ya Jamii ya Tanzania

Authors

  • Anna Nicholaus Kyamba Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Magdaline N. Wafula Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Ushairi, Tanzania, Ukoloni, Uhuru

Abstract

Ushairi wa Kiswahili una historia ndefu kuliko tanzu zote za fasihi andishi ya Kiswahili. Kutokana na historia hiyo, utanzu huu umeweza kutumiwa na waandishi mbalimbali katika kuhifadhi historia ya jamii na taifa kwa ujumla. Wataalamu wengi hasa wa tendi na ushairi mara nyingi hutumia tungo hizo, kueleza visa vya kihistoria. Waandishi walioandika kuhusu tenzi wameweza kuonesha historia nzima ya Tanzania na kutupa picha nzima ya vipindi mbalimbali vilivyopitiwa na Tanzania tangu ukoloni mkongwe na Kiarabu, Kijerumani, uhuru hadi Azimio la Arusha. Hata hivyo, wapo waandishi wengi wa Kiafrika walioandika kazi za ushairi wa Kiswahili, kabla na baada ya uhuru wakionyesha picha halisi iliyokuwepo katika jamii ya Watanzania kipindi hicho na kuonesha historia za watu mashujaa waliopinga udhalimu uliokuwa ukifanywa na wakoloni. Kadhalika, kutokana na uchunguzi wetu wa awali, kupitia ushairi wa Mathias Mnyampala, historia ya taifa la Tanzania imejibainisha zaidi. Mazingira hayo yametuchochea kutafiti zaidi ushairi wa Mnyampala na kuona namna historia ya Tanzania inavyojibainisha kwa uwazi. Hivyo basi, makala haya yanakusudia kuchunguza dhima ya ushairi wa Mnyampala katika kuhifadhi historia ya jamii kwa kuchambua kazi za ushairi za Mnyampala.

Downloads

Published

30-04-2018

Issue

Section

Articles