Kiswahili na Ushairi

Dhima ya Upya wa Kiutunzi

Authors

  • Kemboi Keitany Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Mwanakombo Noordin Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Kiswahili, Ushairi, Dhima, Kiutunzi

Abstract

Kiswahili, kama malighafi ya fasihi, kimekuwa na uwezo wa kuibua upya utunzi wa ushairi wa Kiswahili. Upya huu unaenda sambamba na mabadiliko na hatua zinazopigwa na jamii kadri ya mpito wa wakati. Ni upya unaozidi kunawirisha sanaa ya ushairi wa Kiswahili kiujumi na kiumbuji. Na tunapoangazia upya wa kiutunzi tunazungumzia lugha kama kiungo hai kinachoakisi miktadha halisi ya kihistoria. Licha ya miktadha hii kuathiri mawasiliano ya kawaida ya kila siku ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, inaathiri pia usanii wa kifasihi. Usanii huu wa kifasihi unahusu viambajengo vya kimatini hasa mitindo ya uwasilishaji jumbe. Mitindo hii hudhibitiwa na vipashio vya kimofofonolojia, uradidi wa vipashio vya kiisimu na maumbo badalia ya kileksia yenye uamilifu wa kisintaksia na wa kisemantiki. Uamilifu huu ndio unaoupa ushairi wa Kiswahili upekee wa kiujumi na kiumbuji. Kwa jinsi hiyo, makala haya yanachunguza suala la upya wa kiutunzi kidaikronia katika ushairi wa Kiswahili. Lengo ni kudhihirisha nafasi na uamilifu wa Kiswahili katika kuibua maumbo na mitindo mipya katika utunzi wa mashairi ya Kiswahili.

Downloads

Published

30-09-2018

Issue

Section

Articles