Nafasi ya Nadharia ya Mwingilianotanzu katika Uhakiki wa Fasihi

Authors

  • Fred Wanjala Simiyu Chuo Kikuu Cha Kibabii, Kenya Author

Keywords:

Mwingilianotanzu, Mifanyiko ya Kitanzu, Mwaka Kogwa, Utenguanaji, Usemezano, Mwingiliano wa Kikorasi, Ujinyambuaji na Mwingilianomatini

Abstract

Nadharia ya Mwingilianotanzu inashikilia kuwa, kazi yoyote ya fasihi hujengwa kwa kuvunja mipaka ya kitanzu ili kuibuka na kazi mahuluti. Hii ina maana kuwa, hakuna kazi ya fasihi ambayo inaweza kukamilika bila kuingiliana na kazi nyingine ya fasihi. Malengo makuu ya nadharia hii ni kupinga uchambuzi wa kipweke wa utanzu mmoja mmoja wa fasihi kana kwamba upo utanzu unaoweza kujisimamia kiutendakazi bila kuingiliana na tanzu zingine. Mkabala huu wa kutenganisha tanzu za fasihi ndio ambao umezoeleka katika tafiti na chambuzi nyingi za kazi za fasihi. Mkabala huu unaweka mipaka bayana kati ya tanzu za fasihi kuanzia katika kiwango cha uanishaji. Aidha, utenganishaji huu unaendelezwa pia katika uchanganuzi wa tanzu moja moja za fasihi kana kwamba zinaweza kutekeleza wajibu wake bila kuingiliana na tanzu mbalimbali. Makala hii inathibitisha kuwa uchambuzi wa kazi za fasihi unaweza kufanywa vizuri zaidi kwa kutumia mihimili mahsusi ya nadharia ya Mwingilianotanzu.

Downloads

Published

30-09-2017

Issue

Section

Articles