Usawiri wa Wanaume katika Methali za Kijinsia za Jamii ya Wanyankole
Mtazamo wa Ubabe-Dume
Keywords:
Usawiri, Methali, Kijinsia, Uwezo-UumeAbstract
Makala haya yamechunguza namna wanaume wanavyosawiriwa katika methali za kijinsia, zinavyoweza kujitokeza katika miktadha tofauti ndani ya jamii ya Wanyankole. Mkabala wa kinadharia uliotumika katika uhakiki na uchanganuzi wa data ni nadharia ya Uwezo-Uume. Makala haya yalichunguza na kuhakiki methali za kijinsia katika jamii ya Wanyankole zilizoegemea jinsia ya kiume. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kwamba, jamii ya Wanyankole imekuwa ikitumia methali za kijinsia katika shughuli zake tofauti. Makala haya yamepambanua miktadha za jamii ya Wanyankole zinazoathiri usawiri wa wanaume. Miktadha hizi ni kama ni pamoja na ndoa, utamaduni, malezi na maadili, elimu, uchumi, na uongozi. Mwisho makala haya imebainisha namna na sababu ambavyo methali hizi za kijinsia zilivyowasawiri wanaume katika jamii ya Wanyankole.