Utohozi kama Mkakati wa Mawasiliano katika Mazungumzo kuhusu Ukimwi katika Ekegusii

Authors

  • Carren Nyandiba Chuo Kikuu cha Rongo Author

Keywords:

Utohozi, Mawasiliano, Ukimwi, Ekegusi

Abstract

Tangu kisa cha kwanza cha ukimwi kugunduliwa nchini Kenya, juhudi mbalimbali zimefanywa kujaribu kupunguza idadi ya visa vya maambukizi mapya. Juhudi hizo ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu mbinu na njia mbalimbali za kujikinga dhidi ya maambuki. Elimu kuhusu Virusi vya ukimwi (VVU) na ukimwi hutolewa kwa lugha mbalimbali kutegemea hadhira lengwa. Tafiti zimefanywa kuhusu umuhimu wa lugha katika mawasiliano mbalimbali yakiwemo mawasiliano kuhusu ukimwi.  Mawasiliano kuhusu VVU/ukimwi husheheni mijadala kuhusu sehemu za siri, kitendo cha ngono, matumizi ya kondomu na watu wanaoishi na VVU miongoni mwa mambo mengine. Ingawa mawasiliano ya aina hiyo hufanyika kwa lugha wazi katika Kiingereza, tafiti zimeonyesha kwamba masuala hayo ni mwiko katika baadhi ya lugha za Kiafrika na kwa hivyo hayawezi kujadiliwa kwa lugha wazi. Makala haya yanachunguza utohozi unavyotumka katika mijadala kuhusu VVU/Ukimwi katika lugha ya Ekegusii. Mjadala ambao unajitokeza katika makala haya ulichochewa na sababu kwamba Ekegusii ni mojawapo ya lugha ambazo zimeweka mwiko kwa mazungumzo kuhusu mambo hayo. Aidha, utafiti ulitaka kuchunguza namna lugha ya Ekegusii inakabiliana na suala ambalo limeibuka katika jamii ya sasa. Lengo la Makala haya ni kujadili namna utohozi umetumika katika kujadili sehemu za siri, kitendo cha ngono na matumizi ya kondomu katika diskosi za VVU/Ukimwi.

Downloads

Published

30-04-2018

Issue

Section

Articles