Mtazamo wa Kijumla kuhusu Ushairi wa Kiswahili nchini Kenya

Mifano kutoka Pwani na Bara

Authors

  • Rayya Timammy Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Ushairi, Kenya, Kiswahili, Pwani, Bara, Maudhui, Mtindo

Abstract

Kwa karne nyingi, ushairi umekuwa umekita mizizi katika sehemu za pwani ya Kenya hasa maeneo ya Lamu. Ushairi huu ulifika mpaka sehemu za bara, mahali ambapo Kiswahili kilitumika kusambazia biashara na dini. Hata hivyo, bado hakukuwa na kazi za ushairi za watu wa bara hadi miaka ya kukaribia kipindi cha uhuru katika sehemu za Afrika Mashariki. Japo Kiswahili sasa kinatumika kote nchini Kenya, katika makala hii tuaangalia washairi wa kutoka maeneo haya mawili. Aidha, tutabainisha sifa zinazobainisha ushairi huu wa sehemu hizi mbili; yaani unavyofanana na kutofautiana katika sifa zake za kimaudhui na kimtindo. Vilevile, tutaangalia tofauti za watunzi, lugha wanayoitumia na maswala yanayowashughulisha katika ushairi huu. Mbinu kubwa tuliyotumia ni utafiti wa maktabani uliotuwezesha kupata vitabu na rekodi nyingine. Matokeo muhimu yanabainisha kuwa, washairi wa pwani, hawawezi kuepuka athari ya dini ya Kiislamu katika utunzi wao. Pia, tulibaini kwamba, washairi wa pwani walitumia lahaja zao. Swala lingine muhimu tulilolibaini ni kuwa, washairi wa kike ni wachache sana na hata idadi ya machapisho yao yanapatikana kwa uchache sana nchini Kenya.

Downloads

Published

30-04-2022

Issue

Section

Articles