Tamathali za Usemi na Taswira katika Utenzi wa 'UKIMWI ni Zimwi'
Keywords:
Tamathali, Usemi, Taswira, UtenziAbstract
Utenzi wa UKIMWI ni Zimwi ni kazi iliyotungwa na Mahmoud Abdulkadir wa Lamu katika mwaka wa 2001. Huu ni utenzi ambao mwandishi aliutunga kwa lengo la kuwajuza watu athari za janga la UKIMWI. Utenzi huu umeandikwa katika lahaja ya Kiamu. Maudhui na dhamira ya kazi ya fasihi haziwezi kuwasilishwa na kuwafikia wasomaji bila ya kuwako kwa lugha. Matumizi ya lugha ni mapana kwani huhusisha tamathali za usemi, uteuzi na mpangilio wa maneno basi, sajili za lugha, matumizi ya nahau na misemo n.k. Katika makala haya, ninashughuliki hasa matumizi ya tamathali za usemi na taswira katika utenzi wa UKIMWI ni Zimwi.