Utamaduni Mahuluti katika Ushairi wa Kithaka wa Mberia

Mtazamo wa Baadaukoloni

Authors

  • Samson Ontiri Ongarora Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Utamaduni Mahuluti, Baadaukoloni, Usenge, Elimu ya Kigeni, Ukoloni Mamboleo

Abstract

Kabla ya kuja kwa Waarabu, wamishenari na wakoloni nchini Kenya, Afrika Mashariki na bara la Afrika kwa jumla, wenyeji walikuwa na mila na tamaduni zao. Waarabu, wamishenari na wakoloni walipoingia, tamaduni na mifumo ya maisha ilibadilika. Waarabu walikuja kufanya biashara na kueneza dini ya Kiislamu miongoni mwa wenyeji. Wamishenari vilevile walileta mafunzo mageni kupitia dini ya Kikristo. Baadhi ya wenyeji waliasi tamaduni na mila zao na kupokea mafunzo ya dini ya kigeni. Wakoloni walipokuja, walileta elimu ya kigeni, iliyofundishwa kwa lugha yao; waliendeleza utumwa na kunyakua mashamba licha ya kudhibiti njia kuu za uchumi. Aidha, walileta mifumo mipya ya sheria na kudhihirisha ubaguzi wa rangi kwa sababu ya mila, tamaduni na mienendo yao ya maisha. Kutokana na ujio na maingiliano ya wageni hawa na wenyeji, athari nyingi za kigeni zilianza kuonekana kama vile unyanyasaji wa kiuchumi, unafiki wa kidini, ukahaba na utumwa. Mambo haya yote yalichangia kuibuka kwa utamaduni mahuluti. Vipengele hivi vya utamaduni wa kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni ndivyo vinaonyesha kuwa utamaduni mahuluti unaweza kuwa mzuri na vilevile mbaya. Katika uchanganuzi huu, udhihirishaji wa athari za utamaduni mahuluti katika ushairi wa Kithaka wa Mberia na namna unavyodhihirika katika jamii ya leo umejadiliwa kwa misingi ya nadharia ya baadaukoloni. Katika makala haya, tunachanganua suala la utamaduni mahuluti kama linavyojitokeza katika baadhi ya mashairi ya Kithaka wa Mberia katika diwani za Mchezo wa Karata (1997), Bara Jingine (2001), Redio na Mwezi (2005) na Msimu wa Tisa (2007).

Downloads

Published

30-09-2021

Issue

Section

Articles