Usawiri wa Wanawake wenye Uwezo katika Muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania
Keywords:
Mkabala wa Ulinganishi, Kizazi Kipya, Bongo Fleva, Uhusiano wa KijinsiaAbstract
Kwa kutumia mkabala wa ulinganishi, makala haya yanajadili uhusiano wa kijinsia unaobainishwa katika muktadha ambao mwanamke ndiye mmiliki wa mali na ambaye ana fursa katika vyombo vya kufanya maamuzi. Tafiti nyingi zinazungumzia suala la ujinsia zikijikita katika kumwangalia mwanamke kama chombo kinachotumiwa na wanaume katika kutimiza matakwa yao. Pia, zinasawiri namna mwanamke anavyozingirwa na mfumo usio mpa fursa za uhuru binafsi pamoja na maendeleo. Makala haya yanalenga kuleta ukengeushi wa suala hili, kwa kumtazama mwanamke ambaye ana uwezo wa kimaendeleo, mathalani uwezo wa kielimu, kiuchumi, kisiasa, na hata kushiriki katika vyombo vya maamuzi, jinsi ambavyo uhusiano wake ndani ya jamii unavyosawiriwa. Kwa kutumia nyimbo za muziki wa bongo fleva, kama fasihi simulizi pendwa nchini Tanzania, makala yatajadili mahusiano yake na jinsia nyingine na hata na jamii kwa ujumla. Katika makala haya, ulinganishi wa nyimbo za mziki wa bongo fleva zilizoimbwa na jinsia tofauti utafanyika.