Siasa, Uchumi na Ustawi wa Jamii
Mtazamo wa Kisemiotiki wa Ushairi wa Kivumba
Keywords:
Ushairi, Siasa, Uchumi, Ustawi, Kivumba, Semiotiki, Kiishara, KirejeleziAbstract
Makala hii inachunguza nafasi ya ushairi katika kuzungumzia masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni pamoja na ustawi wa jamii kupitia ushairi wa Kivumba. Ili kukuza mjadala wetu, makala hii ilifafanua ishara na maana katika ushairi wa Kivumba kwa kutumia nadharia ya semiotiki kutumia misimbo ya Barthes. Lengo la mjadala wetu ni kubainisha ya kwamba, ushairi unaweza kuwa chombo mbadala cha kuzungumzia masuala yanayoikumba jamii kikamilifu. Makala hii inazingatia kauli kwamba, malighafi makuu ya fasihi simulizi ni jamii. Makala hii inajadili kwamba, sio rahisi kufasiri ishara na maana katika ushairi wa jamii yoyote nje ya mkutadha wa jamii yenyewe. Ili kuongoza mjadala huu, mjadala ulijikita katika ushairi wa Kivumba pekee kwa kutumia misimbo mitano ya Barthes. Ushahidi wote uliotegemewa katika mjadala wetu ni ule uliotokana na mifano iliyokusanywa kutoka nyanjani katika maeneo ambapo Kivumba kinazungumzwa nchini Kenya baina ya 1919-2020.