Uchanganuzi wa Vigezo Vinavyotumika Kuwajenga Wahusika katika Ushairi wa Kiswahili

Authors

  • Baraka Sikuomba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author
  • Joviet Bulaya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Wahusika, Ushairi, Kiswahili, Seif Khatib

Abstract

Makala hii imechunguza vigezo vilivyotumiwa kuwajenga wahusika katika ushairi wa Kiswahili. Makala hii imetokana na madai ya tafiti kueleza kwamba mashairi mengi andishi hayana wahusika bali mashairi simulizi (Samwel, Selemani na Kabiero; 2013). Kutokana na madai hayo tuliona ipo haja kuchunguza vigezo vinavyotumika kuwajenga wahusika katika ushairi andishi wa Kiswahili pamoja na wahusika waliojengwa kupitia vigezo hivyo. Ili kutimiza azma ya makala hii, utafiti umefanywa kwa kurejelea diwani tatu, yaani Fungate ya Uhuru (1988), Wasakatonge (2003) na Vifaru Weusi (2016). Data za msingi za makala hii zilipatikana maktabani kwa mbinu ya usomaji matini na uchambuzi wa nyaraka. Kadhalika, katika makala hii Nadharia ya Uhalisia ndiyo iliyoongoza mchakato mzima wa uwasilishaji na uchambuzi wa data. Matokeo ya utafiti yaliyozaa makala hii yameonesha vigezo kama vile kigezo cha kitaswira, kigezo cha usimulizi, kigezo cha kifasihi simulizi na kigezo cha kiishara ndivyo vilivyotumiwa na mwandishi Seif Khatib kuwajenga wahusika katika diwani teule. Pia, makala hii imeonesha kila kigezo kilivyotumika kuwajenga wahusika katika ushairi wa Kiswahili kupitia diwani teule za makala hii. Makala hii inapendekeza kufanyika kwa tafiti nyingine katika fasihi andishi zitakazotofautisha na kulinganisha vigezo vinavyotumika kuwajenga wahusika wa ushairi na tanzu nyingine za fasihi andishi kama vile riwaya, tamthiliya na hadithi fupi.

Downloads

Published

30-09-2023

Issue

Section

Articles