Athari za Ulumbilugha Miongoni mwa 'Chokoraa'

Authors

  • Ruth M. Binyanya Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • Ayub Mukhwana Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • Samuel M. Obuchi Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Ulumbilugha, Lugha Mkakati, 'Chokoraa'

Abstract

Makala haya yanachunguza athari za ulumbilugha katika kutimiza nia za wakati husika za Chokoraa. Chokoraahutumia lugha mbalimbali katika mawasiliano yao. Uteuzi wa lugha itakayotumiwa na Chokoraa hutegemea muktadha maalum. Chokoraa hutumia Kiswahili, Sheng’, Kiingereza na lugha za asili katika mazungumzo yao. Ulumbilugha ndio huwafanya Chokoraa wakati mwingine kuchanganya ndimi kwa kutumia lugha ambazo wanazijua huku wakitaka kutimiza nia mahsusi. Kwa hali hii basi tunaweza kusema kuwa wanaulumbilugha huteua lugha kwa mujibu wa muktadha kutokana na ukweli kuwa lugha moja yaweza kuwa faafu katika muktadha mmoja na wala sio mwingine. Pia, makala haya yanaainisha athari za ulumbilugha kama zinavyojitokeza katika mazungumzo ya Chokoraa wa mtaa duni wa Mathare, jijini Nairobi.

Downloads

Published

30-09-2020

Issue

Section

Articles