Sheng kama Lugha ya Biashara jijini Nairobi
Masiala ya Kijamii Yanayoathiri Nafasi yake katika Utangaziaji wa Biashara
Keywords:
Utangaziaji, Biashara, Mazungumzo, Nadharia ya MchezoAbstract
Sheng ni lugha kipindi chini Kenya ambayo imeenea katika utangaziaji wa biashara mbalimbali jijini Nairobi kwa sababu ni lugha pendwa nchini Kenya hasa miongoni mwa vijana na ambao ndio walio wengi. Vijana wengi jijini Nairobi hutumia Sheng na kuiona kama lugha inayowapa ujitambulishaji, mvuto wa kiujumisia na ubunifu wa aina yake hasa inapotumika katika utangaziaji wa biashara jijini Nairobi. Sheng pia imeonekana kutumiwa na wauzaji bidhaa walio na sifa tofauti tofauti za kijamii kama vile umri na jinsia ili kuivutia hadhira lengwa na kujitambulisha nayo. Lengo kuu la makala haya ni kubainisha masiala ya kijamii yanayoathiri nafasi ya Sheng katika utangaziaji wa biashara jijini Nairobi. Hii ni kutokana na hali kwamba katika karne hii Sheng imetagaa kimatumizi jijini Nairobi hasa katika utangaziaji wa biashara mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa. Data kwa ajili ya Makala haya ilikusanywa na mtafiti kwa kutumia hojaji, mahojiano na uchunguzi shiriki. Watafitiwa 80 ambao ni wauzaji bidhaa walichaguliwa kimaksudi na kushirikishwa. Nadharia ya Maafikiano ya Mawasiliano iliyoasisiwa na Giles na Wenzake (1970) na Nadharia ya Mchezo iliyoasisiwa na John von Nuemann na Oskar Morgentern (1944) pamoja na mikondo ya hivi karibuni kuzihusu nadharia hizi zilitumiwa katika uchanganuzi wa data. Matokeo tuliyopata yameonyesha kuwa kunayo masiala mbalimbali ya kijamii ambayo huathiri matumizi ya Sheng katika utangaziaji wa biashara jijini Nairobi. Miongoni mwayo kukiwepo jinsia, umatabaka, viwango vya elimu, umri na mahali pa makazi ya wahusika jijini Nairobi.