'Sipangwingwi, Watajua Hawajui'
Jaribio la Kuelekeza Matumizi ya Lugha Dhidi ya Uhalisia wa Kiisimujamii
Keywords:
Sipangwingwi, Watajua, HawajuiAbstract
Makala haya yanaangazia nyimbo mbili, ‘Sipangwingwi’ na ‘Watajua hawajui’ ambamo mnapatikana maneno mawili Sipangwingwi na Watajua hawajui. Hivi karibuni, Serikali ya Kenya, kupitia Shirika la NCIC imetoa tamko ambalo linaharamisha matumizi ya haya maneno mawili, miongoni mwa mengine kwa madai kwamba huenda yanaweza kuibua hisia fulani ambazo zinaweza kuchangia hali ya machafuko katika na baina ya Jamii-tumizi lugha mbalimbali. Makala haya basi yanajadili matumizi ya vifungu hivi viwili kwa kurejelea nyimbo hizo mbili ambapo waandishi wamejaribu kuonyesha kwamba ni makosa kuelekeza matumizi ya lugha, kwa kuwalazimisha wanajamii kutotumia maneno fulani ambayo, huenda yanatumiwa kwa wingi na mtu au mwanasiasa fulani. Ukweli wa kiisimujamii ni kwamba, lugha inafaa kujiendeleza, kujikuza na kujisambaza kote, kutegemea watumiaji wake, katika muktadha wowote: sokoni, kanisani, msikitini, mtaani, na kwingineko.