Mwingiliano wa Kisimulizi katika Tenzi za 'Fumo Liyongo' (UFL), 'Gilgamesh' (UG), 'Mikidadi na Mayasa' (UMM) pamoja na 'Simulizi ya Samsoni' (SS)

Authors

  • Priscah J. Kiprotich Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Samuel M. Obuchi Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Mwanakombo Mohamed Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Mwingilianomatini, Usimulizi, Tenzi, Biblia, Waamuzi

Abstract

Makala haya yanajadili suala la mwingilianomatini katika tendi teule na matini ya kidini. Mabadiliko katika jamii yanayoletwa na teknolojia ya kisasa yamesababisha baadhi ya kazi za kijadi kama vile tenzi, kusahaulika. Tenzi ni hifadhi muhimu ya historia ya jamii, hivyo zinafaa kuhifadhiwa kwa kufanyiwa utafiti zaidi ili ziendelee kuwa na manufaa katika jamii. Kutokana na udurusu wa maandishi uliofanywa na watafiti, ilidhihirika kwamba tenzi za Fumo Liyongo (UFL), Gilgamesh (UG), Mikidadi na Mayasa (UMM) pamoja na Simulizi ya Samsoni (SS) zinawasilisha visa mbalimbali kwa njia ya usimulizi. Matini hizi teule zina mwangwi fulani unaohisika kisimulizi. Makala haya yamezingatia Biblia kama matini muhimu ambayo ina wingi wa kazi za kifasihi zinazohitaji kuhakikiwa, mojawapo ikiwa Simulizi ya Samsoni. Makala haya yamejadili mbinu za kisanii zilizotumika kisimulizi ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa.

Downloads

Published

30-04-2021

Issue

Section

Articles