Kiswahili kama Lugha Changizi

Uchambuzi wa Kifonolojia wa Maneno Yaliyokopeshwa Lugha ya Kikikuyu

Authors

  • P. I. Iribemwangi Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Ukopaji, Maneno Mkopo, Utohozi, Chanzo, Ushabaha, Kifonolojia, Kiswahili, Kikikuyu

Abstract

Ukopaji katika lugha hupelekea kukua kwa lugha inayokopa. Kwa sababu hiyo, ukopaji ni mchakato uendeleao aushi. Kwa hakika, kila lugha ambayo wazungumzaji wake wamewahi kutagusana na wazungumzaji wa lugha nyingine haiwezi kuepuka maneno ya mkopo. Kutokana na masiala haya, tafiti nyingi zimefanywa kuhusu ukopaji na utohozi. Jambo linalodhirika ni kwamba mkazo huwekwa katika lugha pokezi huko lugha changizi ikipuuzwa. Kiswahili ni mojawapo wa lugha zinazosemwa kukopa sana hadi kuitwa lugha chotara na baadhi ya wasomi. Hata hivyo, jambo ambalo halijatiliwa mkazo ni kwamba Kiswahili nacho kimechangia katika kukuza msamiati wa lugha nyingi duniani. Hii leo, kuna maneno kadhaa ya Kiswahili hata katika lugha zilizosambaa sana kama Kiingereza. Kikikuyu ni mojawapo ya lugha zilizokopa maneno mengi kutoka Kiswahili. Watumizi wa Kiswahili na Kikikuyu wamekuwa na mtagusano hadi mwanzo wa karne iliyopita. Kutokana na hali hiyo, ukopaji unadhihirika. Makala haya yanachanganua mbinu tofauti za kifonolojia zinazotumika katika kutohoa maneno ya Kiswahili yanapoingia katika Kikikuyu. Kwa kuwa Kikikuyu kina lahaja zipatazo tano tofauti, katika kuchunguza maneno hayo, makala makala haya yatachota kutoka kwa lahaja hizo zote. Makala yatatumia mwelekeo wa Mshabaha-Chanzo wa Utohozi wa Manenomkopo (Source-Similarity Model of Loanwords Adaptation) ambao ni mmojawapo wa mielekeo ya Nadharia ya Ulinganifu (Correspondence Theory). Mwelekeo huu husisistiza kuwepo kwa mshabaha/ulinganifu mkubwa baina ya neno asilia na neno linalokopwa. Kwa kutumia mwelekeo huu, makala yanaonyesha kwamba mbinu zinazotumiwa kwa maneno yanayokopeshwa ni pamoja na udondoshaji, udumishaji, ubadilishaji pamoja na uhamishaji wa konsonanti. Kwa upande mwingine, mbinu za utohozi zinazotumiwa kwa irabu ni kama vile uchopekaji, udumishaji na ubadilishaji. Mbinu hizi huhakikisha kuwa maneno mkopo yanashabihiana kwa kiasi kikubwa na yale asilia ya Kiswahili.

Downloads

Published

30-04-2019

Issue

Section

Articles