Ukubalifu wa Silabi Funge katika Fonolojia ya Kiswahili

Authors

  • David Majariwa Chuo Kikuu cha Kabale Author

Keywords:

Ukubalifu, Uwekevu wa Nguvu, Umbo Upeo, Ufonolojishaji

Abstract

Makala haya yanachunguza ukubalifu wa silabi funge katika fonolojia ya Kiswahili kwa kutumia mifano kutoka Kiarabu na Kiingereza. Tafiti kadhaa zilibainisha uchopezi wa irabu baada ya konsonanti funge kuwa ni mkakati wa urekebishaji unaotumiwa sana katika upokeaji wa maneno ya mkopo katika Kiswahili ili kuondoa silabi funge. Hata hivyo silabi funge zimebainika katika fonolojia ya Kiswahili. Kutokana na msingi kuwa mifumo ya fonolojia ya lugha hufikiriwa kuwa thabiti zaidi dhidi ya mabadiliko, kuna haja ya kuchunguza ukubalifu wa silabi funge hizo katika fonolojia ya Kiswahili. Data zilizotumika zilipatikana kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu 2013 (KKS), Toleo la tatu. Nadharia ya Umbo Upeo sambamba na Nadharria ya fonolojia Amirifu zilitumiwa katika uchanganuzi wa data. Matokeo yanaonesha kuwa upangiliaji upya wa mashartizuizi unaeleza upenyezaji wa silabi funge katika Kiswahili na ukubalifu wa silabi funge hizo umeelezwa na fonolojia Amirifu. Uelekeo wa watumiaji wa lugha ya Kiswahili kutumia nguvu kwa uwekevu katika matumizi ya ala za matamshi umesababisha fonolojia ya Kiswahili kuzuia uchopezi wa irabu katika upokeaji wa maneno yenye silabi funge kutoka Kiingereza na Kiarabu.

Downloads

Published

30-09-2021

Issue

Section

Articles