Matatizo ya Tafsiri katika Kazi za Fasihi
Tajriba Yangu Kutokana na Tafsiri ya 'Othello-Tanzia ya Mtu Mweusi'
Keywords:
Tafsiri, Fasihi Tafsiri, Matatizo ya Tafsiri, OthelloAbstract
Tamthilia ya Othello ni moja katika tamthilia pendwa za mwandishi maarufu wa Kimagharibi William Shakespeare. Othello ni moja katika tamthilia chache za Shakespeare zilizotafsiriwa kwa Kiswahili. Tamthilia zingine za Shakespeare zilizotafsiriwa kwa Kiswahili ni Juliasi Kaizari na Mabepari wa Venisi zote na Mwalimu Julius Nyerere. Makala haya yanahoji kwamba uchache wa tafsiri za vitabu vya Shakespeare unatokana na matatizo ya tafsiri yanayomkumba mtafsiri katika shughuli ya tafsiri. Lengo la makala haya ni kubaini matatizo ya tafsiri yanayomkumba mtafsiri wa kazi za fasihi kwa kurejelea tafsiri ya Kiswahili ya tamthilia ya Othello.