Juhudi za Kukabiliana na Kuangamia kwa Lugha za Kiafrika

Authors

  • S. M. Obuchi Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Kifo cha Lugha, Kuhatarishwa kwa Lugha, , Sera ya Lugha

Abstract

Dhana ya kuhatarishwa kwa lugha imejadiliwa ndani ya muktadha wa dhana ya kufa kwa lugha. Hivyo, makala yamezijadili sababu mbalimbali zinazipelekea lugha, kuhatarishwa, na hatimaye kufa. Dhana za kuhatarishwa na kufa kwa lugha zimejadiliwa kwa pamoja kwa sababu zinasababishana, yaani, ya kwanza inapotokea, uwezekano wa ya pili kutokea ni yakini. Makala yamerejelea takwimu ambazo zinaonyesha kwamba zaidi 50% ya lugha zilizoko ulimwenguni huenda zikahatarishwa na kutoweka kufikia 2100. Hii ni kutokana na sababu za kiuchumi, kisiasa, kisera, hali kadhalika, kuhamia lugha kuu na changamoto ya kuibuka na kuongezeka kwa miji. Hali hii huweza kusababisha wasemaji wa lugha ndogondogo kuhamia lugha kuu kwa ajili ya kusaka kazi. Makala yameonyesha namna lugha hizo zilizo hatarini zinavyoweza kuokolewa, kutokana na juhudi za kisera.

Downloads

Published

30-09-2019

Issue

Section

Articles