Kikale cha Kifo kama Mbinu ya Utunzi katika Fasihi ya Kiswahili
Keywords:
Kifo, Kikale, Tanzia, Tamthilia ya KiswahiliAbstract
Makala haya yanachunguza tukio la hatima ya maisha ya kifo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likidhihirika na kutumiwa na watunzi katika kazi za sanaa hususani tamthilia. Kifo ni taashira kongwe ambayo imekuwepo katika kazi za sanaa za jamii zote ulimwenguni na katika vizazi na ustaarabu wa nyakati mbalimbali. Kifo kama kikale kimekuwa kikijitokeza mara kwa mara katika kazi za sanaa kwa njia ya kujirudia rudia kiasi kwamba kinajibainisha kama motifu ya utunzi wa kazi za fasihi inayoathiri muundo na dhamira za kazi hizo. Matokeo ya uchunguzi yanafafanua matumizi ya kifo kama mbinu ya utunzi wa tamthilia ya Kiswahili na kudhihirisha kifo kama kikale kinachojirudiarudia katika kazi za fasihi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhakiki wa vikale iliyoasisiwa na mtaalamu Northrop Frye (1957) kutoka Kanada.