Usilahaishaji Lugha katika Intaneti kama Tisho kwa Umoja wa Kitaifa

Authors

  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Mahero Toboso Chuo Kikuu Kishirikishi cha Alupe Author

Keywords:

Usilahaishaji, Lugha, Intaneti, Teknolojia

Abstract

Kwa muda mrefu, lugha imekuwa ikitambulika kama ala ya kimsingi ya kufikiria, kufanikisha mawasiliano, kutambulisha, kuwasilisha utamaduni na katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hata hivyo, maendeleo ya kisiasa na uvumbuzi wa teknolojia mpya za mawasiliano ulimwenguni yameleta mielekeo mipya katika matumizi ya lugha. Sasa, lugha inatumiwa kwa njia zinazoidhihirisha na kuibainisha kama silaha ya kudhuru au hata kuangamiza. Katika historia ya mataifa, lugha imetumiwa katika maeneo mbalimbali katika kuanzisha vita, kuhujumu na hata kushawishi watu kufanya uhalifu. Kuzuka kwa intaneti kumesababisha kuibuka kwa mielekeo mipya ya usilahaishaji wa lugha. Majukwaa ya Twitter, Facebook, Instagram, Telegram na Whatsapp yamewapa watumizi wa mitandao hii fursa ya kutumia lugha kwa njia za kibunifu na kusababisha usilahaishaji wa lugha kwa njia za kipekee. Tafiti zimefanywa kuhusu uhalifu wa mitandaoni. Hata hivyo, suala la lugha na usilahaishaji wake halijashughulikiwa kwa dhati na kwa umuhimu unaostahili. Makala haya yanashughulikia usilahaishaji wa lugha katika majukwaa ya mitandao ya kijamii. Imebainika kwamba uhuru wa matumizi ya lugha katika mitandao hii umesababisha matumizi mabaya ya lugha.

Downloads

Published

30-06-2019

Issue

Section

Articles