Lugha za Kienyeji kama Kizingiti cha Kuleta Umoja wa Kitaifa na Uwiano Barani Afrika

Authors

  • Basilio Gichobi Mungania Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Lugha Enyeji, Lugha Rasmi, Lugha ya Taifa, Lugha Mawasiliano

Abstract

Lugha ni chombo muhimu sana katika kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa na wa kieneo. Katika taifa la Kenya na kanda ya Afrika ya Mashariki, hakuna lugha iliyo na uwezo wa kuleta mshikamano na muungano tunaoutamani isipokuwa Kiswahili. Kiswahili kina wajibu mkubwa wa kuchangia mshikamano wa kitaifa na wa kikanda. Hata hivyo, lugha hii inakumbwa na changamoto nyingi katika kutekeleza wajibu huu adimu, zikiwemo zile za kijamii, kiuchumi, na za kisiasa. Mojawapo ya changamoto kubwa inatokana na lugha za kiasili ambazo huwa ni kikwazo kikubwa kutokana na kutumiwa kwazo na wananchi wengi katika mataifa mengi ya Afrika ya Mashariki. Lugha za kiasili hutumiwa kwa wingi sana katika mataifa mengi ya Afrika ya Mashariki, hususan katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Ni katika nchi ya Tanzania pekee ambapo Kiswahili hutumiwa ipasavyo na ndiposa nchi hiyo inaakisi muungano wa kitaifa. Makala haya yatatathmini jinsi lugha ya Kiswahili inavyoweza kutumiwa kama wenzo wa kuchangia katika kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa na wa kikanda pamoja na changamoto zinazokikumba Kiswahili katika wajibu wake wa kuleta umoja wa kitaifa na wa kikanda. Zaidi itachanganua ushindani unaotokana na lugha enyeji.

Downloads

Published

30-06-2019

Issue

Section

Articles