Vipashio vya Lugha Vinavyosawiri Ubabedume katika Majigambo ya 'Miviga ya Shilembe' na 'Mchezasili wa Mayo' Miongoni mwa Waisukha Nchini Kenya

Authors

  • Mary Lukamika Kibigo Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro Author
  • Susan C. Choge Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro Author
  • Fred Wanjala Simiyu Chuo Kikuu cha Kibabii Author

Keywords:

Ubabedume, Majigambo Shilembe, Mayo, Waisukha

Abstract

Makala haya yanahusu dhana ya ubabedume katika majigambo ya miviga ya Shilembe na mchezasili wa Mayomiongoni mwa Waisukha nchini Kenya. Utafiti huu ulihakiki vipashio mahsusi vya lugha kwa mtazamo wa kisemantiki ili kubainisha jinsi vinavyosawiri na kuendeleza ubabedume katika miviga ya Shilembe na mchezasili waMayo. Makala yalihakiki majigambo kumi na sita yaliyokusanywa kwa kutumia uchunzaji-shirikishi, usaili, unasaji na ujazaji wa hojaji. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa, lugha ya majigambo ya miviga ya Shilembe na Mchezasili wa Mayo yamedhihirisha kuwa, masuala ya kijamii yanasawiriwa kisanii kupitia mwingiliano-taaluma kati ya fasihi na isimu. Utafiti umeonyesha kuwa, lugha ni kipawa ambacho jamii hutumia wakati mwingine vibaya kumtukuza mwanamume zaidi na kumpa uwezo na mamlaka juu ya mwanamke.

Downloads

Published

30-09-2019

Issue

Section

Articles