Nafasi ya Sitiari katika Mabadiliko ya Kisemantiki ya Leksia za Kiswahili
Ulinganisho wa Kiswahili cha Kabla ya Karne ya Ishirini na Kiswahili cha Kisasa
Keywords:
Sitiari, Mabadiliko, Semantiki, LeksiaAbstract
Makala haya yamejadili nafasi ya sitiari katika mabadiliko ya kisemantiki ya leksia za Kiswahili kwa kulinganisha mifano mahususi ya Kiswahili cha kabla ya Karne ya Ishirini na Kiswahili cha Karne ya Ishirini na Moja. Aidha, imeshughulikia mahusiano kati ya maana za leksia za awali na za kisasa. Makala pia imejadili athari za sitiari katika muundo wa lugha ya Kiswahili. Asili ya data iliyochanganuliwa ni kutoka kwa matini teule za kabla ya Karne ya Ishirini na kutoka kwa wazungumzaji wenye elimu-asilia. Uchanganuzi umeonyesha bayana kuwa mbinu ya sitiari imekuwa muhimu katika kubadilisha maana za leksia na pia muundo wa kisemantiki wa Kiswahili, katika kipindi kilichotafitiwa. Pindi jamii nzima ilivyobadilika kutokana na maendeleo ya sayansi, teknolojia, uchumi, kijamii na kisiasa, ndivyo pia lugha ya sitiari mpya zinazidi kuchipuka.