Mitandao ya Kijamii na Mabadiliko ya Kiswahili katika Karne ya Ishirini na Moja

Authors

  • Kenyani Sangili Chuo Kikuu cha Rongo Author

Keywords:

Mabadiliko ya Lugha, Kijamii, Mtandao

Abstract

Wanafalsafa wa kale walidai kuwa, duniani, hakuna kitu ambacho hakikosi kubadilika. Mojawapo ya vitu vinavyobadilika ni lugha. Lugha za binadamu hubadilika katika kila kizazi kwa sababu mbalimbali za kiisimujamii na kiteknolojia. Kwa kuwa lugha za binadamu ni kitu changamano, mabadiliko yake hutokea kwa matawi ya kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia, kisemantiki na kipragmatiki. Kuna sauti ambazo hutoweka katika lugha, na zingine hukopwa. Maana za leksimu hupanuka au hufinyika kutegemea matumizi yake kimuktadha. Kwa njia hii, mawasiliano ya binadamu huathirika kwani mabadiliko ya lugha hubadilisha mawasiliano na jinsi washiriki wanavyofasiri maana za kauli. Utafiti huu ulichunguza mabadiliko ya lugha ya Kiswahili mintarafu mitandao ya kijamii. Hii ni kwa sababu mojawapo ya vitu vinavyosababisha lugha kubadilika katika karne ya 21 ni teknolojia.

Downloads

Published

30-04-2017

Issue

Section

Articles