Mtagusano wa Uforensiki na Riwaya ya Kiswahili
Mfano kutoka Riwaya ya ‘Mzimu wa Watu wa Kale’
Keywords:
Mtagusano, Forensiki, Teknolojia, Fasihi, RiwayaAbstract
Makala haya yanahusu mtagusano wa uforensiki katika riwaya ya Kiswahili. Pia, yanaonesha namna taaluma ya uforensiki inavyojitokeza katika riwaya ya Kiswahili na kuonesha mtagusano ambao umejenga maudhui na fani katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale kwa kujikita katika vipengele vya: wahusika, msuko wa matukio, muktadha, matumizi ya lugha, mgogoro na mtindo wa usimulizi wa kiforensiki. Aidha, makala haya yanatambulisha uhusiano uliopo kati ya taaluma ya Uforensiki na Fasihi katika kufikisha ujumbe kwa jamii husika. Makala haya yatatumia nadharia ya mwingiliano matini ambayo itasaidia kuweka bayana namna taaluma ya uforensiki inavyojitokeza katika riwaya ya Kiswahili. Makala haya pia, yataibua tafakuri mpya ya riwaya ya Kiswahili na uforensiki itakayoleta chachu kwa wanataaluma na wahakiki wa kazi za fasihi katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia.