Dhima ya Viakifishi katika Ushairi Huru wa Kiswahili

Authors

  • Joseph Nyehita Maitaria Chuo Kikuu cha Karatina Author

Keywords:

Dhima, Viakifishi, Ushairi Huru

Abstract

Ushairi, kama zilivyo tanzu nyingine za fasihi, huwasilishwa kwa matini za lugha zilizoakifishwa ili kuelekeza usomaji, uwasilishaji wa kimantiki, kubainisha zaidi matini zilizotumika na kuondoa utata katika fasiri za jumbe kusudiwa. Washairi hutumia viakifishi kama mtindo na mbinu ya kibinafsi katika uwasilishaji. Hata hivyo, kuna aina mbili za matumizi ya viakifishi katika uwasilishaji wa tanzu za fasihi: Kwanza kuna matumizi ya ‘kawaida’ ambayo ni utaratibu unaofahamika miongoni mwa watunzi. Aghalabu matumizi haya yanajitokeza zaidi katika tungo za mashairi zinazingatia mno arudhi katika uwasilishaji. Pili, kuna matumizi ya ‘makusudi’ ya viakifishi ambayo yanabainika zaidi katika uwasilishaji wa mashairi ya Kiswahili yanayowasilishwa kwa kutozingatia mno arudhi za utunzi. Kutokana na uwepo wa njia hizo mbili za uwakifishaji, kuna haja ya kufafanua na kufasiri dhima ya viakifishi katika ushairi wa Kiswahili. Makala hii inafafanua namna watunzi wa ushairi huru wa Kiswahili wanavyotumia viakifishi kama mtindo na mbinu elekezi katika kuwasilisha hisi, ubainishaji wa ujumbe na ujenzi wa muktadha wa usomaji. Mifano itatokana na baadhi ya mashairi katika diwani za Kichomi (E. Kezilahabi) na Bara Jingine (K. Wa Mberia). Mwishowe, imependekezwa namna viakifishi vinavyoweza kutumiwa kwa ufaafu zaidi katika uelekezaji wa taratibu za usomaji na uwasilishaji wa ujumbe katika mashairi ya Kiswahili.

Downloads

Published

30-09-2017

Issue

Section

Articles