Usimulizi katika Ushairi wa Kithaka wa Mberia
Keywords:
Usimulizi, Usimulizi wa Nafsi ya Kwanza, Usimulizi wa Nafsi ya Pili, Usimulizi MwakoteAbstract
Kithaka wa Mberia ni mtunzi wa mashairi huru. Ametunga diwani kadhaa za mashairi huru yenye maudhui anuwai na masuala ibuka. Katika kuangazia maudhui mbalimbali katika ushairi wake, ametumia mbinu ya usimulizi katika baadhi ya mashairi katika diwani zake. Usimulizi unatumika sana katika utambaji wa hadithi katika fasihi simulizi na katika tanzu za riwaya na hadithi fupi katika fasihi andishi. Ni nadra sana usimulizi kutumika katika ushairi. Ingawa tenzi ndizo zinahusishwa na usimulizi kama vile katika Utenzi wa Fumo Liyongo (1913), inawezekana mashairi mafupi yakawa na sifa ya usimulizi kama tunavyoona katika mashairi ya Kithaka wa Mberia. Katika makala haya, tunajadili aina za usimulizi katika baadhi ya mashairi yake katika diwani zake nne ambazo ni: Mchezo wa Karata (1997), Bara Jingine (2001), Redio na Mwezi (2005), na Rangi ya Anga (2014). Matumizi haya ya mtindo wa usimulizi ndiyo yanayoupa ushairi wake ubunifu mpya, usasa na upekee fulani.