Usayansi wa Miiko ya Waafrika na Uhalisia wake kwa Jamii ya Kileo

Mifano Kutoka Jamii ya Wapare

Authors

  • Hatibu Sadi Chuo Kikuu cha Rongo Author
  • James Ontieri Chuo Kikuu cha Rongo Author
  • Tigiti S. Y. Sengo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Author

Keywords:

Miiko, Usayansi, Waafrika, Jamii

Abstract

Makala haya yanahusu usayansi wa miiko ya Waafrika na uhalisia wake kwa jamii ya kileo. Mifano iliyorejelewa ni ya jamii ya Wapare wa Mwanga mkoani Kilimanjaro. Kutokana na dhima muhimu ya miiko katika ustawi wa jamii kimaadili, makala haya yanakusudia kuweka bayana usayansi wa miiko ya Wapare. Jambo hilo ni muhimu kwa kuwa, linashadidia hoja ya kuwa jamii haiwezi kutenganishwa na miiko kutokana na mwingiliano wa moja kwa moja kati ya jamii na miiko hiyo. Toka jadi, miiko imekuwa na dhima adhimu ya kusimamia maisha ya wanadamu kwa kuendeleza maadili yanayoiwezesha jamii kuishi kwa namna bora. Uzoefu unaonesha kuwa, miiko na jamii ni vitu visivyoweza kutenganishwa. Kwa hali hiyo, jamii isiyo na miiko haipo. Data kwa ajili ya makala haya zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili huru na uchambuzi wa matini. Mbinu hizo ziliwawezesha watafiti kupata taarifa nyingi kuhusu usayansi unaodhihirika kwenye miiko na uhalisia wake. Nadharia ya Taalimu ina Kwao na Fasihi ina Kwao, ndio iliyotumiwa kwenye mwendelezo wa uchunguzi na uchambuzi wa makala haya. Matokeo ya utafiti wa makala haya yalionesha kuwa, miiko ya jamii ina uhalisia kwenye maisha ya jamii ya kileo kutokana na dhima zake. Pia ilibainika kuwa, miiko ina misingi madhubuti ya kisayansi na hivyo kudhihirisha mantiki kuwa, iliwekwa baada ya kufanyiwa tathmini na kuonekana kuwa ni ya muhimu. Kwa hali hiyo, jamii za Kiafrika zinahimizwa kuendeleza miiko yenye manufaa kwa jamii zao ili kuimarisha maisha ya kila siku.

Downloads

Published

30-04-2024

Issue

Section

Articles