Methali za Kiswahili katika Kukabiliana na Ufisadi nchini Kenya

Authors

  • Joseph Nyehita Maitaria Chuo Kikuu cha Karatina Author

Keywords:

Methali za Kiswahili, Ufisadi, Athari

Abstract

Kero za ufisadi (kwa sasa) zimekuwa zikigonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari na kuzungumziwa kila uchao nchini Kenya. Visa hivyo vimezagaa na vingali vinarindima katika maisha ya watu. Wananchi wanaonyesha dalili za kusinywa na vitendo hivyo na wamekuwa wakiitaka serikali kutoa adhabu kali zaidi kwa wote wanaoendeleza visa hivyo. Suala hili limekuwa likiwapiga ngeo wananchi; wanaposhuhudia wale wanaonaswa au kuhusishwa katika vitendo hivyo; hufikishwa mahakamani na kutokea milango wa nyuma. Hili si jambo la mzaha; inaashiria kuwa, matumizi ya nguvu hayajafua dafu na hazijawa mwafaka kama njia ya kukabiliana na janga la ufisadi.  Athari ya ufisadi nchini Kenya zi tele; mshikamano wa watu unaendelea kumomonyoka, akina yakhe nao hawana cha kutumaini wala kutegemea na wanaendelea kumasikinishwa; nazo fedha za umma zinazotokana na ushuru zinaendelea kupotea pote! Makala haya yanajaribu kuelezea namna methali za Kiswahili zinavyobainisha sura mbalimbali za ufisadi kwa azma ya kuwaongoza wanajamii katika kujenga mikakati ya kukabiliana na janga hilo nchini Kenya kwa wakati wa sasa.

Downloads

Published

30-04-2018

Issue

Section

Articles