Ufundishaji wa Fasihi-Tafsiriwa kwa Kiswahili katika Vyuo Vikuu nchini Kenya
Keywords:
Ufundishaji, Fasihi-Tafsiriwa, KiswahiliAbstract
Fasihi-tafsiriwa zinafunzwa katika idara za Kiswahili za vyuo vikuu nchini Kenya. Aidha, zimekuwa zikifuzwa kama mojawapo ya kozi za lazima au ya hiari. Baadhi ya wanafunzi huliendeleza somo hili kwa kufanyia utafiti katika shahada ya uzamili na uzamifu. Kozi hii hufundishwa kama kozi inayojisimamia au baadhi ya vitabu teule hujumuishwa katika kozi za fasihi ya Kiswahili. Swali ni, malengo ya kufundisha kozi hizi ni yepi katika idara za Kiswahili za vyuo vikuu? Aghalabu mafunzo hayo hugusia zaidi maudhui yanayowasilishwa na kunga zalizotumiwa katika uwasilishaji. Azma ya makala hii ni kutathmini namna fasihi-tafsiriwa ya kigeni inavyofuzwa katika Idara za Kiswahili katika vyuo vikuu nchini Kenya. Kadhalika, imependekezwa namna ufunzaji huo unavyoweza kuelekezwa zaidi katika kukabiliana na upungufu uliopo.