Mchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili

Uchunguzi wa Riwaya ya 'Mafuta'

Authors

  • Simiyu Benson Sululu Chuo Kikuu cha Kibabii Author
  • Richard Makhanu Wafula Chuo Kikuu cha Kenyatta Author
  • Joseph Nyehita Maitaria Chuo Kikuu cha Karatina Author

Keywords:

Waswahili, Riwaya ya Kiswahili, Tanzu za Kimaigizo, Unyumbufu, Umahuluti

Abstract

Riwaya ni mojawapo ya tanzu za fasihi andishi ambazo zimepiga hatua kimaendeleo katika uandishi wake. Mathalan, riwaya ya Kiswahili imeandikwa na waandishi ambao ni Waswahili na ambao si Waswahili. Kwa hivyo, riwaya ya Kiswahili inaeleza tajriba ya Waswahili na Waafrika wengine wasiokuwa Waswahili. Mazingira wanamotoka waaandishi wa riwaya ya Kiswahili, wasiokuwa Waswahili, yamechangia na kuathiri uandishi wao. Waandishi hawa wameingiza vipengele vya fasihi simulizi na utamaduni wa jamii zao katika riwaya za Kiswahili wanazoandika. Makala haya yanalenga kuchunguza jinsi uingizaji wa vipengele hivi vya fasihi simulizi za watunzi wa riwaya ya Kiswahili, wasiokuwa Waswahili, unachangia umahuluti wa riwaya hii. Mahsusi, makala haya yamedadavua mchango wa tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi katika umahuluti wa riwaya ya Kiswahili kupitia mfano ya riwaya ya Mafuta iliyoandikwa na Katama Mkangi. Uchunguzi huu umefanywa kwa kutumia Nadharia ya Umahuluti wa Utamaduni inayoshikilia kwamba panapotokea hali ya mtagusano baina ya tamaduni tofauti, matokeo yake si wingi-tamaduni bali ni mchanganyiko wa vipengele kutoka tamaduni hizi ambao zao lake huwa na sifa za kimahuluti. Nadharia hii imetumiwa kufafanua jinsi umahuluti wa riwaya ya Kiswahili umechangiwa na uingizaji wa vipengele vya tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi kutoka jamii ya mtunzi teule ambaye si Mswahili. Katika kufanya hivyo, makala haya yamebainisha jinsi riwaya ya Kiswahili ilivyo nyumbufu kwa ambavyo inajumuisha vipengele kutoka asili anuai ambavyo vinaifanya kuwa changamano na ya kimahuluti.

Downloads

Published

30-09-2021

Issue

Section

Articles