Ushairi Huru wa Kiswahili Utashuka Lini?
Keywords:
Ushairi, Kiswahili, Historia, MustakabaliAbstract
Makala haya yanafafanua mustakabali wa mashairi huru ya Kiswahili katika muktadha wa historia ya Ushairi wa Kiswahili. Mashairi yanayowasilishwa kwa kuzingatia arudhi za kimapokeo yamekuwepo na yana hadhira kubwa katika mataifa ya Afrika ya Mashariki hadi sasa. Mwishoni mwa miaka ya 1950 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1960, mashairi yasiyozingatia mno arudhi za kimapokeo ‘yalijitokeza’. Awali, watunzi wa mashairi haya waliwapa kibarua kigumu wakereketwa na walezi wa mashairi hayo. Hivyo, kulikuwa na jitihada za kutoa maelezo yanayohitajika kuhusu mihimili muhimu katika tasnia ya ushairi wa Kiswahili. Watunzi wa ushairi huru katika miaka ya 1960 hadi 1980 walikuwa ni vijana waliobahatika kupata elimu ya darasani na kujipatia shahada katika masuala ya tahakiki za fasihi za Afrika Mashariki na kutoka sehemu nyingine ulimwenguni. Hivyo, waliotoa maelezo kuhusu ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia taratibu za uhakiki wa kinadharia. Wataalamu na isimu na wahakiki wa fasihi waliunga mkono mawazo hayo. Kadhalika, wasomi na wahakiki wa fasihi ya Kiswahili (hasa katika vyuo vikuu); mashairi hayo yamekuwa ni ‘vito’. Kwa kuzingatia uwapo wamashairi huru na ya kimapokeo ni yapi yenye hadhira pana? Makala haya yanafafanua uhalisi unayoyafanya tungo za mashairi ya Kiswahili kuwa maarufu au kutokuwa maarufu katika jamii ya sasa.