Mbinu, Dhima na Athari za Kumuanika Nje Mfiwa katika Utendaji wa Utani wa Wahehe

Authors

  • Asifiwe Asifiwe Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author
  • Edith B. Lyimo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Utani, Utendaji, Kuanika, Mfiwa, Dhima, Athari

Abstract

Utani ni kipera cha mazungumzo/nyambi katika fasihi simulizi chenye dhima mbalimbali kwa jamii husika. Lengo la makala hii ni kuchunguza mbinu, dhima na athari za kumuanika nje mfiwa katika utendaji wa utani wa Wahehe. Maswali tunayojibu ni: Je, ni utani upi unaojitokeza wakati wa kumuanika nje mfiwa? Nini dhima na athari ya utendaji huo wa utani kupitia mbinu ya kumuanika nje mfiwa? Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano na ushuhudiaji wa misiba na kuchambuliwa kwa kutumia Nadharia ya Utendaji na Uamilifu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa mbinu ya kumuanika nje mfiwa pindi anapopatwa na msiba hufuata hatua kadhaa wakati wa utendaji wa utani. Utendaji wa utani huo kupitia mbinu ya kumuanika nje mfiwa huwa na dhima kama vile; kudumisha umoja na ushirikiano, kupunguza majonzi kwa wafiwa, kuilinda amali hii muhimu ya utani miongoni mwa wanajamii, kuonya na kuburudisha. Makala hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu; utangulizi, kiini na hitimisho. Utangulizi unaeleza kwa ujumla dhana ya utani pamoja na nadharia zilizotumika. Kiini kinaelezea mbinu, dhima na athari za kumuanika nje mfiwa katika utendaji wa utani wa Wahehe. Sehemu hii imefuatiwa na mbinu za kiutendaji wa utani wakati wa kumuanika nje mfiwa, dhima, athari zake na mwisho hitimisho.

Downloads

Published

30-04-2022

Issue

Section

Articles