Mwingiliano Matini kama Kunga ya Uandishi katika Riwaya za S.A Mohamed
"Dunia Yao" (2006) na "Nyuso za Mwanamke" (2010)
Keywords:
Ubaadausasa, MwingilianomatiniAbstract
Makala haya yameshughulikia mwingilianomatini kama kunga ya uandishi katika riwaya mbili za S.A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010) zilizondikwa katika mwongo wa kwanza wa K21. Riwaya hizi zinaonekana kuwa changamano zikilinganishwa na riwaya za kimapokeo kwa kugeukia mtindo wa uandishi wa ubaadausasa. Makala haya yaliongozwa na nadharia ya ubaadausasa inayopendekeza uanuwai katika kueleza tajriba tofauti za binadamu. Uchanganuzi ulibaini kuwa riwaya hizi zina matumizi mengi ya mwingilianomatini yaliyojikita katika matini mbalimbali zikiwemo za kifasihi, kidini, kihistoria na kifalsafa. Makala haya yamedhihirisha kuwa matumizi ya mwingilianomatini ni mbinu ya kiumbuji ambayo mwandishi ameitumia kuendeleza dhamira mbalimbali zinazoathiri ulimwengu katika K21. Hata hivyo imebainika kuwa riwaya hizi huenda zikaitenga hadhira isiyobobea katika fani mbalimbali za kijamii na aghalabu huleta ugumu wa kufuatilia dhamira mbalimbali zinazojitokeza katika kazi hizi.