Urudiaji wa Kisimulizi na wa Kisemantiki kama Mtindo katika Tenzi
Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari Bin Darimi
Keywords:
Utenzi, Umitindo, Uchimuzi, Urudiaji wa Kisimulizi, Urudiaji wa Kisemantiki, Urudiaji wa Kiesajesia, Urudiaji wa SemikiAbstract
Riwaya na tamthilia kama tanzu za fasihi ya Kiswahili ni mazao ya karne ya ishirini, tofauti na utenzi ambao uliandikwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1570. Sifa moja kuu tena ya kimsingi katika utanzu wa ushairi hasa utenzi ni matumizi ya urudiaji wa kisimulizi na ule wa kisemantiki. Sifa ya urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki ambayo ni wazi kabisa katika maisha ya binadamu ina utata wake unaotokea katika vipengele mbalimbali. Urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki hutokea katika viwango mbalimbali na vipengele hivyo ndivyo kiini cha fani na maudhui. Licha ya kazi na umuhimu wa urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki katika tenzi za Kiswahili, kwa uelewa wetu hakuna uhakiki wa kina ambao umefanywa katika vipengele hivi, licha ya utenzi kuchunguzwa sana. Yaliyomo ni mambo ya kijumla kuhusu urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki ambayo hayajaangazia majukumu na umuhimu huo. Kazi nyingi zimekosa kuhakiki kwa kina urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki kama mtindo katika ushairi. Kwa hivyo, katika makala haya, lengo letu limekuwa kujadili kwa kina urudiaji wa kisimulizi na wa kisemantiki kama mtindo unaofanikisha fani na maudhui katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi.