Uchanganuzi Linganishi wa Suala la Maadili kwa Vijana wa Kiume katika Tenzi Mbili

'Siraji' na 'Adili'

Authors

  • Gwako Bosibori Jackline Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • Rayya Timammy Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Maadili, Tenzi, Mafunzo

Abstract

Makala hii imeshughulikia maadili kwa vijana wa kiume yanayojitokeza katika tenzi za Siraji na Adili. Katika uchunguzi huu tumeongozwa na nadharia ya maadili ambayo inalenga kazi za fasihi kutatua matatizo ya jamii kwa njia ipasavyo na kujenga jamii bora yenye maelewano. Malengo ya uchunguzi wetu ni kulinganisha jinsi ambavyo watunzi Kijumwa na Robert wamelishughulikia suala la maadili kwa vijana wa kiume katika tenzi Siraji na Adili na hatimaye kubaini sababu za kuwiana kwao. Baada ya kusoma na kuzichambua tenzi- Siraji na Adili tumebaini ya kwamba watunzi Kijumwa na Robert wamewiana kwa jinsi wamelishughulikia suala la maadili kwa vijana wa kiume. Tumeweza kuonyesha kwamba tenzi hizi zina uhusiano wa karibu sana kwa sababu watunzi Kijumwa na Robert wameyafungamanisha maadili hayo na mafunzo ya dini ya Kiislamu ndiposa tukachanganua data yetu kwa njia ya maelezo na ufafanuzi huku tukitoa thibitisho kutoka kwa tenzi- Siraji na Adili pamoja na Kurani Takatifu. Ni matumaini yetu kwamba makala haya yatachangia pakubwa katika taaluma ya kiusomi kwa kuendeleza fasihi andishi.

Downloads

Published

30-09-2017

Issue

Section

Articles