Tahakiki Linganishi ya Motifu Zinazobainika katika Tendi za 'Mikidadi na Mayasa' na 'Kalevala'
Keywords:
Motifu, Tendi, Jaala, Ruwaza ya ShujaaAbstract
Mjadala na mgogoro mkali mno katika jamii ya usomi. Hii ni kutokana na rai kuwa wasomi na watafiti wengi kutoka maeneo ya Kimagharibi walidai kuwa Afrika hakuna tendi ila kinachodaiwa kuitwa tendi ni masimulizi ya kisifo tu. Suala la motifu katika kazi ya fasihi ni la kimsingi mno kwani hubainisha ni kwa kiwango kipi vipengele mbalimbali vya kifasihi huingiliana na huonyesha ni kwa njia zipi ambapo kazi ya fasihi hurudiarudia dhana mbalimbali ili kuleta msisitizo na kukuza maudhui pamoja na dhamira. Ili kujaribu kutatua mzozo na utata uliopo kuhusu uwepo wa tendi katika maeneo ya Kiafrika, Makala haya yalichunguza iwapo motifu zinazobainika katika tendi za maeneo haya mawili zinawiana au la. Madhumuni makuu yalikuwa kutathmini iwapo kuna mwingiliano na mfanano wa motifu mbalimbali baina ya tendi za Kiafrika na zile za Kimagharibi. Waandishi walichunguza tendi mbili zinazopatikana katika maeneo ya Kiafrika na Kimagharibi. Tendi hizi ni Utendi wa Mikidadi na Mayasa (Afrika) na Utendi wa Kalevala (Finland).