Fasihi ya Watoto ya Kiswahili na Mshikamano wa Kitaifa
Keywords:
Fasihi ya Watoto, Utaifa, MshikamanoAbstract
Makala haya yanabainisha nafasi ya Fasihi ya Watoto katika mshikamano wa kitaifa. Waandishi wamerejelea vitabu teule vya fasihi ya watoto ambavyo ni Urembo wa Ngiri (2016) na Sungura Mpanda Ngazi (2008). Mshikamano wa kitaifa nchini Kenya umekuwa ukitikiswa hasa kutoka mwaka wa 2007/2008 wakati ghasia zilizuka baada ya Uchaguzi Mkuu. Tangu wakati huo wameibuka waandishi wapya wanaoandikia masual ya fasihi ya watoto ambayo licha ya kuburudisha ina dhima na mielekeo mipya inayolenga kukuza utaifa na mshikamano. Makala haya yanalenga kuthibitisha kuwa fasihi ya watoto imechukua mielekeo mipya ambapo, sawia na fasihi ya watu wazima, inatekeleza dhima muhimu katika uhamasisho wa kisiasa na mshikamano wa kijamii.