Vyanzo vya Mitengo ya Wahusika Mashujaa katika Tungo za Kitendi za Kiswahili

Uchunguzi wa Riwaya-Tendi ya 'Siri Sirini'

Authors

  • Neema Benson Sway Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author
  • Shani Omari Mchepange Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Mitengo, Wahusika Mashujaa, Tungo za Kitendi

Abstract

Kifasihi, mitengo (umoja ‘mtengo’) inajumuisha kutengwa na kujitenga kwa wahusika mashujaa katika muktadha wa kisaikolojia, kiutendaji na kimazingira (Hegel, 1949; Seeman, 1959; Durkheim, 1964; Chiduo na wenzake, 2016). Utokeaji wake katika namna mbalimbali umefanya hata vyanzo vyake kuwa ni mahuluti, mintarafu ya tafiti zilizopo ambazo zimejikita zaidi katika mitengo ya kimazingira (Propp, 1968; Kunene, 1985; Senkoro, 1997; Michaux, 2003). Suala hili ndilo limechochea makala hii ambayo inachunguza vyanzo vya ujitokezaji wa mitengo mbalimbali ya wahusika mashujaa kupitia utungo wa Siri Sirini. Nadharia ya Mtengo na Mkabala wa Kitaamuli umetumika kuchanganua data za utafiti huu. Vyanzo vilivyobainika kusababisha mitengo ya wahusika mashujaa ni pamoja na suala la hofu ya kiongozi mkuu kwa shujaa, shujaa kutoridhishwa na utendaji wa kisiasa, mwito binafsi wa shujaa kitaifa, utanguzi wa miiko ya kimila na shujaa kukwepa uhasama wa kiakraba. Makala imepanua maarifa kuhusu mambo yanayoibua mitengo ya wahusika mashujaa wa tungo za kitendi, kwani imefanikiwa kujumuisha vyanzo mbalimbali vinavyosababisha mitengo ya namna zote (ya kijiografia, kiutendaji na kisaikolojia) kwa ujumla wake. Matokeo yamepanua pia ufafanuzi wa dhana hii ya mitengo katika fasihi na imetambulisha ufaafu wa nadharia ya ‘Mtengo’ katika uchambuzi wa kazi za kifasihi.

Downloads

Published

30-09-2022

Issue

Section

Articles