Uamilifu wa Taashira katika Tamthilia za 'Zilizala' na 'Sudana'

Authors

  • Waithiru Kago Chuo Kikuu cha Laikipia Author
  • Wendo Nabea Chuo Kikuu cha Laikipia Author
  • James Ogola Onyango Chuo Kikuu cha Laikipia Author

Keywords:

Taashira, Miundomsingi, Watawala, Vikaragosi, Utandawazi

Abstract

Makala haya yanahusu matumizi na uamilifu wa taashira katika tamthilia za Zilizala na Sudana. Katika makala haya matumizi ya taashira yalichunguzwa kupitia vyombo vya usafiri, hali za kimaumbile na miundomsingi. Makala haya yaliyojikita katika nadharia ya baada ya ukoloni yanaonyesha kuwa taashira imetumika katika tamthilia zilizopo kama mbinu ya kusana mambo yanayoathiri kitovu cha jamii. Haya ni pamoja na viongozi wa kiimla, ufisadi, ukabila na ubinafsi. Aidha, yanaeleza kuwa taashira imetumika vyema katika tamthilia hizi madhali imesaidia waandishi kuepuka uwezekano wa kusawiri masuala yanayokumba jamii paruwanja, jambo ambalo lingenyima kazi zenyewe mvuto. Badala yake imeonyeshwa kuwa waandishi walifinyanga lugha na kuyasawiri masuala ya kawaida kwa namna ngeni na ya kutendesa kupitia taashira. Yanadhihirisha tadi na inda zinazotumiwa na baadhi ya watawala katika mataifa yanayoinuka kiuchumi kujinufaisha kibinafsi pamoja na vikaragosi wao. Isitoshe, makala haya yamedhihirisha jinsi viongozi wa mataifa hayo hudhibitiwa na watawala katika mataifa yaliyoinuka kiuchumi na kusababisha ufukara wa raia katika mahusiano yanayofichika katika istilahi ya kitasfida ya utandawazi.

Downloads

Published

30-04-2021

Issue

Section

Articles