Mikakati ya Kudumisha Hejemonia katika Siasa na Uchumi: Mfano wa Riwaya za 'Dharau ya Ini', 'Msimu wa Vipepeo', 'Msururu wa Usaliti' na 'Majilio ya Mkombozi'
Keywords:
Hejemonia, Mahejemoni, Mikakati ya Kudumisha Hejemonia, Safu ya HejemoniaAbstract
Makala haya yanaangazia suala mikakati ya udumishaji wa hejemonia katika siasa na uchumi kama inavyodhihirika katika riwaya teule za Kiswahili. Makala haya yanachunguza ufanifu wa mikakati inayotumiwa na mabwanyenye kuendeleza na kudumisha hejemonia mintarafu ya riwaya za Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usalitina Majilio ya Mkombozi. Mihimili ya nadharia ya hejemonia inayofafanua jinsi watawala hudumisha utawala wao kwa kutumia mikakati mbalimbali ilitumika katika kuhakiki data. Aidha makala haya yanatoa hamasisho kwa wanajamii kuhusu mikakati inayotumiwa na viongozi kuwashawishi raia waendelee kuunga mkono utawala uliopo hususan katika hali ambapo kihalisia wanafaa kuukosoa na kuupinga.