Mielekeo ya Lugha na Ruwaza za Matumizi ya Lugha ya Walimu wa Kiswahili wa Shule za Msingi katika Kaunti ya Siaya
Keywords:
Mielekeo ya Lugha, Ruwaza za Matumizi, Kiswahili, Lugha na JamiiAbstract
Makala haya yalichunguza na kubainisha mielekeo ya walimu wa Kiswahili katika shule za msingi za kaunti ya Siaya. Aidha, ruwaza zao za matumizi ya lugha zilipambanuliwa. Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji. Wasailiwa 34 waliteuliwa kutoka kaunti ndogo sita za kaunti ya Siaya. Data ilichanganuliwa kwa mkabala mseto kwa kutumia njia za kitakwimu na kimaelezo. Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kupitia njia za maelezo na majedwali. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba walimu walikuwa na mielekeo kubalifu kuhusu Kiswahili. Aidha, ruwaza za matumizi yao ya lugha zilidhihirisha kwamba matumizi ya Kiswahili yamezidi kupanuka katika mawanda mengi ya kijamii katika Kaunti ya Siaya.