Changamoto za Kuunda Programu Tumizi ya 'Kikagua-Tahajia' ya Lugha za “Runyačitara”
Keywords:
'Kikagua-Tahajia', Changamoto, Maneno Mnasaba, Mofofonolojia, Othografia, “Runyačitara”Abstract
Makala haya yanafafanua changamaoto za kuunda programu tumizi ya kikagua-tahajia cha lugha za “Runyačitara”. Kwa kuwa lugha za “Runyačitara” ni lugha ambishi bainishi, maumbo ya maneno na uchanganuzi wake kimofolojia ni changamani. Uchangamani huu unafafanuliwa na namna unavyozua changamoto za kiothografia, kimofolojia na kileksika katika mchakato wa kuandaa kikagua-tahajia. Data kutoka uwandani na maktabani imechambuliwa kwa kutumia mbinu linganishi. Imebainika kwamba ili maneno yaweze kutumiwa katika mchakato wa kukagua-tahajia, kuna haja ya kuunda kamusi ya leksimu ambayo itaingizwa kweye kompyuta, kuelezea othografia, ruwaza na kanuni za undaji wa maneno na sarufi maumbo ya lugha za “Runyačitara” kwa ujumla. Katika kufanya hivyo, makala haya yanabaini kwamba ingawa kuna maneno mnasaba, kuna changamoto za kimofofonolojia na za kileksika katika maneno ya lugha hizi. Kwa miundo inayofanana kanuni za kuandaa maneno kwa ajili ya kikagua- tahajia zimependekezwa.